WATANZANIA MSIWE NA WASI WASI HAKUNA MGONJWA WA HOMA YA NYANI NCHINI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 3 August 2022

WATANZANIA MSIWE NA WASI WASI HAKUNA MGONJWA WA HOMA YA NYANI NCHINI



Mganga Mkuu wa serikali Dr.Aifello Sichwale amewatoa hofu watanzania juu ya taarifa za uwepo wa ugonjwa wa homa ya nyani katika maeneo mbalimbali duniani ambapo amesema hadi sasa hakuna mgonjwa wa homa hiyo hapa nchini.


Akizungumza na wataalamu wa afya wilaya ya Babati mkoani Manyara Dr. Sichwale amesema kumekuwa na maswali mengi yanayoonyesha hofu kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa homa ya nyani,ambapo amesema serikali inafuatulia kwa ukaribu taarifa za Kila mgeni anayeingja nchini.


Amesema serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo ufuatiliaji wa wasafiri wanaoingia nchini kupitia vituo vyote vya mpakani na tayari watumishi wamepatiwa mafunzo ya utambuzi wa ugonjwa huo.


Ugonjwa wa homa ya Nyani husababishwa na wanyama aina ya Nyani na Panya ambapo mgonjwa huwa na mwonekano wa malengelenge hasa maeneo ya mkono yanayofanana na ugonjwa wa Tetekuwanga.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso