MZEE WA MIAKA 59 AJIUA KWA KUJINYONGA KWA SHUKA GESTI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 3 August 2022

MZEE WA MIAKA 59 AJIUA KWA KUJINYONGA KWA SHUKA GESTI





Mzee mwenye umri wa miaka 59, Msham Omary Mpulu mkazi wa Tandika Jijini Dar es salaam ambaye alikuwa fundi selemala amejinyonga hadi kufa katika nyumba ya kulala wageni maeneo ya Somanga wilayani Kilwa mkoani Pwani.


Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Pwani, ACP Marco Chilya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo inadaiwa marehemu alichukua uamuzi huo baada ya kukabiliwa na madeni.


Kamanda Chilya amesema tukio hilo limetokea mnamo Agosti 1, 2022 ambapo mwili wa marehemu ulikutwa katika nyumba ya kulala wageni iitwayo KIJUMBI katika maeneo ya Somanga ambapo wahudumu wa nyumba hiyo asubuhi walimgongea mlango bila mafanikio ya marehemu kufungua hivyo waliamua kuvunja mlango.


Amesema baada ya kuvunja mlango walimkuta marehemu amefariki ambapo alijitundika kwenye dirisha kwa kutumia shuka na ndugu wa marehemu wamethibitisha kuwa chanzo ni ndugu yao kukabiliwa na madeni mengi.

CHANZO:GLOBALTV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso