KAHAMA: NGAYIWA AKAGUA MIRADI YA MILIONI 48 SHULE YA MSINGI KOROGWE. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 5 August 2026

KAHAMA: NGAYIWA AKAGUA MIRADI YA MILIONI 48 SHULE YA MSINGI KOROGWE.

 



Na Nyamiti A, Nyamiti.


Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Mh. Benjamin Ngayiwa amesema atashirikiana na wataalam wa idara ili kutatua changamoto ya vyoo vya walimu, ukosefu wa mashine ya Photocopy kwa ajili ya kuandalia mitihani, changamoto ya Umeme Shule ya Msingi Korogwe, kata ya Malunga Manispaa kahama Mkoani Shinyanga.


Ahadi hiyo ameitoa Agosti 5 wakati wa mkutano wa wazazi na walezi uliofanyika shuleni, Baada ya kusikia changamoto hizi kutoka kwa Afisa Elimu wa Kata, Matrida Tunge Masuke, akitoa taarifa ya Elimu katika shule hiyo.


katika ziara hiyo ya kukagua miradi ya maendeleo ya elimu Ngayiwa amesema shule hiyo imenufaika na ujenzi wa madarasa 3 mapya ambapo madarasa 2 tayari yameezekwa kwa gharama ya Tsh. Milioni 8 fedha ya mfuko wa jimbo na madara 3 kukarabatiwa kwa Tsh mil 40.


Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Malunga, Mh. Ahmed Haruna amesema wananchi wa kata hiyo wako tayari kushirikiana na Serikali katika sekta mbalimbali za maendeleo nakuongeza kuwa Malunga ni miongoni mwa wanufaika wa fedha za Serikali katika miradi ya elimu na miundombinu ya barabara inayotekelezwa.


Wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo wamemuomba Mh. Ngayiwa kuendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto nyingine ndani ya kata na jimbo ikiwemo ukamilishaji wa miradi ya nguvu za wananchi, tatizo la kukatika kwa maji na miundombinu ya barabara.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso