CHANZO AJALI YA BAGAMOYO ILIYOUA WATU 9, DEREVA WA LORI KU-'OVERTAKE' - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 11 March 2024

CHANZO AJALI YA BAGAMOYO ILIYOUA WATU 9, DEREVA WA LORI KU-'OVERTAKE'

Watu tisa wamefariki katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Kiromo Jana usiku, March 10, 2024 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani baada ya Coaster ya Abiria ikitokea Dar es salaam kuelekea Bagamoyo kugongana uso kwa uso na Lori lililobeba mawe likitokea Bagamoyo kuelekea Dar es salaam.


Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge  amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori kutaka kulipita gari jingine bila kuchukua tahadhari.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Halima Okash amewapa pole Wananchi wa Bagamoyo na kuwashukuru Wananchi wa Kiromo kwa kutoa msaada kwa Majeruhi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso