SIWEZI KUJIUNGA CCM - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 11 March 2024

SIWEZI KUJIUNGA CCM

Mwenyekiti mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Juma Duni Haji amesema hawezi kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.


Akizungumza Machi 10, 2024 visiwani Zanzibar, Juma Duni ‘Babu’ amesema atafia ndani ya ACT na kwa sababu hiyo yupo tayari kutoa ushirikiano wake kwa chama hicho.



“Nimemsikia Mbeto (Khamis Mbeto, Katibu Mwenezi, CCM Zanzibar kuwa ananikaribisha CCM. Naomba leo nimjibu kuwa Mimi siwezi kwenda CCM.” Amesema Juma Duni.


Juma Duni amesema baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa chama hicho, kilichobaki ni kuwaunga mkono viongozi waliopewa dhamana ya kukiongoza cha hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso