MARUBANI WALIOLALA WAKIWA ANGANI KWA DAKIKA 28 WACHUNGUZWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 11 March 2024

MARUBANI WALIOLALA WAKIWA ANGANI KWA DAKIKA 28 WACHUNGUZWA

Indonesia inaichunguza kisa cha marubani wawili kupatikana wakiwa wamelala kwa dakika 28 katikati ya safari ya ndege ya Batik Air iliyokuwa ikifanya safari kutoka Sulawesi kwenda Mji Mkuu Jakarta nchini humo.

Marubani ambao wote wawili wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, wanadaiwa kuhusika katika tukio hilo Januari 25, 2024, ambapo mmoja wao aliripotiwa kuchoka kutokana na kusaidia kuwatunza watoto wake pacha wachanga.

Ndege hiyo aina ya Airbus A320 iliacha njia kwa muda, lakini ikatua salama, huku abiria wote 153 na wahudumu wote wakiwa salama, limeripoti Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Marubani hao ambao hawakutajwa majina mmoja mwenye umri wa miaka 32 alimwambia mwenzake (28) kuwa achukue udhibiti wa ndege hiyo takribani nusu saa baada ya kupaa, akisema alihitaji kupumzika kidogo, lakini rubani msaidizi naye alilala pia bila kukusudia kwa mujibu wa ripoti ya wizara ya uchukuzi, alipitiwa na usingizi.

Mamlaka za udhibiti wa anga ya Jakarta zilijaribu kuwasiliana na chumba cha marubani cha ndege hiyo bila mafanikio baada ya mawasiliano yao ya mwisho kurekodiwa.

Kimya hicho cha redio kilidumu kwa dakika 28 hadi rubani kiongozi alipoamka na kugundua kuwa mwenzake naye alikuwa amepitiwa na usingizi. Pia aligundua kuwa ndege hiyo ilikuwa imeacha njia kwa muda mfupi.

Kisha marubani waliitikia wito kutoka Jakarta na kufanikiwa kutua salama.

Uchunguzi wa kimatibabu kabla ya safari hiyo ulibaini kuwa marubani hao walikuwa wana afya inayofaa kusafirisha abiria.
Shinikizo lao la damu na mapigo ya moyo yalikuwa ya kawaida na hawakuwa na dalili zozote za utumiaji pombe.

Mwaka 2019 ndege ya shirika hilohilo ililazimika kutua kwa dharura baada ya rubani wake mwingine kuzirai akiwa safarini.
  • mwananchi_official's profile picture

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso