WATU WATANO WAFARIKI KAGONGWA NA 18 WABAINIKA KUWA NA KIPINDUPINDU SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 9 January 2024

WATU WATANO WAFARIKI KAGONGWA NA 18 WABAINIKA KUWA NA KIPINDUPINDU SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema jumla ya wagonjwa 18 kati ya wagonjwa 41 wameathirika na vimelea vya kuhara na kutapika Mkoani Shinyanga.




Na Mapuli Misalaba


Ameyasema hayo leo Jumanne Januari 9,2024 wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya ugonjwa wa kuhara na kutapika ulioibuka hivi karibuni na kusadikiwa vifo vya watu watano katika kata ya Kagonjwa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga.


Amesema wagonjwa 41 kati yao 18 wamebainika kuathirika na vimelea vya ugonjwa wa kuhara na kutapika katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Shinyanga.


RC Mndeme ameeleza kuwa tayari Mkoa umeunda timu maalumu ya kuratibu na kufuatilia mwenendo wa ugonjwa huo ambapo mpaka sasa zipo kambi tatu za kufanya matibabu ya ugonjwa huo ambazo ni kituo cha Afya Ihapa katika Manispaa ya Shinyanga, kituo cha Afya Kagongwa Manispaa ya Kahama na kituo cha Afya Kishapu Halmashauri ya Kishapu.


“Mnamo tarehe 28.12.2023 Mkoa wetu katika kata ya Kagongwa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama vilitokea vifo 5 ambavyo vilisababishwa na kuhara na kutapika, hali hiyo ilipelekea Mkoa kufanya ufuatiliaji katika eneo la Kagongwa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga”.


“Mkoa umeunda timu ndogo ya wataalam ya kuratibu na kufuatilia mwenendo wa ugongwa huu ambayo tayari imeanza kazi, aidha kwa kila Halmashauri timu kama hizi zimeundwa na kusimamiwa kikamilifu ili kuzuia kusambaa na kuenea kwa ugonjwa huu hatari”.


“Mpaka sasa tunakambi tatu za kufanya matibabu ya ugonjwa huo ambazi ni kituo cha Afya Ihapa katika Manispaa ya Shinyanga, kituo cha Afya Kagongwa Manispaa ya Kahama na kituo cha Afya Kishapu Halmashauri ya Kishapu”.amesema RC Mndeme


Amesema wagonjwa 30 tayari wameruhusiwa ambapo mpaka sasa wagonjwa watano (5) bado wanaendelea na matibabu kwenye vituo na kwamba kituo cha afya katika Manispaa ya Kahama wapo wagonjwa wwili, kituo cha Afya Kishapu wapo wagonjwa wawili na kituo cha afya Ihapa Manispaa ya Shinyanga yupo mgonjwa mmoja.


Mhe. Mndeme amefafaua kuwa mpaka sasa hakuna vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Kipindupindu na kwamba vifo vya watu waanne (4) wametoka kwenye jamii na mtu mmoja amefariki akiwa katika Zahanati binafsi ambapo wote hawakufanyiwa vipimo.


“Kwa kifupi ugonjwa wa kuhara na kutapika husababishwa na watu kula Kinyesi kibichi kupitia vyakula au vinywaji na kuenezwa kwa haraka na hivyo huweza kusambaa kwa muda mfupi zaidi”.


“Dalili za ugonjwa huu ni kama vile kuharisha mfululizo na mgonjwa kuishiwa maji mwilini ugonjwa huu huenezwa kwa njia ya kutumia maji yasiyochemshwa, kula matunda bila kuosha na maji masafi na tiririka, kula chakula cha baridi au kiporo, matumizi hafifu ya vyoo, utunzaji mbaya wa vyakula pamoja na usafi duni wa mazingira”.


“Ugonjwa huu unawea kuepukika kwa kutumia maji safi na salama, kuepuka kula vyakula vilivyopoa, kutumia maji yaliyotiwa dawa ya Aqwa tabs pamoja na matumizi sahihi ya vyoo bora”.amesema RC Mndeme


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ametaja shughuli zinazoendelea kutolewa katika kuhakikisha Mkoa unakuwa salama ili kujikinga na ugonjwa huu ikiwemo upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa ajili ya kutolea huduma kwa wananchi, kuhakikisha wahisiwa wanafuatiliwa pamoja na ndugu au waliokuwa pamoja na wagonjwa (contacts).


Amesema mikakati mingine inayotumika ni pamoja na kutoa elimu juu ya namna nzuri ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kuhara na kutapika, kutumia wahudumu wa Afya ngazi ya jamii kutembele kaya na kutoa elimu ya namna nzuri ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kuhara na kutapika, kufanya vipimo vya maji katika visima mbalimbali katika Halmashauri zilizoathirika na ugonjwa a kuhara na kutapika, kuwasafirisha wagonjwa kutoka maeneo yao ya awali kwenda katika vituo vya matibabu pamoja na kutoa huduma za tiba kwa waliogundulika kuwa n ugonjwa huu.

CHANZO:MISALABA MEDIA

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso