ADAIWA KUJINYONGA BAADA YA MWENZA WAKE KUCHUKULIWA NA WAZAZI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 18 January 2024

ADAIWA KUJINYONGA BAADA YA MWENZA WAKE KUCHUKULIWA NA WAZAZI

Mkazi wa Mtaa wa Idundilanga, wilayani Njombe, Venance Haule (24) anadaiwa kujinyonga kwa kile kinachoelezwa mwanamke aliyekuwa akiishi naye kuchukuliwa na wazazi wake wakati bado anampenda.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga, ameeleza hayo leo Januari 18, 2024 alipozungumza na waandishi wa habari na kusema Haule amejinyonga kwa kutumia pazia chumbani kwake.


Amesema tukio hilo limetokea jana, Januari 17, 2024 asubuhi na inadaiwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na ndugu wa mwanamke huyo wakishinikiza amlipie mahari kwa vitisho kuwa ni mwanafunzi.


Kamanda Banga amesema mwanamke aliyekuwa akiishi na marehemu huyo alikuwa mwanafunzi, aliacha shule mwaka 2023 akiwa kidato cha tatu.


“Mwaka 2024 alitakiwa kuwa kidato cha nne, lakini kwa kutokuwepo shuleni kwa muda mrefu walimfukuza, kwa hiyo si mwanafunzi tena,” amesema Banga.


Amesema kulingana na maelezo ya mwanamke aliyekuwa akiishi na marehemu ni kuwa ndugu zake walikuwa wanakwenda kwa mwanamume huyo kujitambulisha kuwa wao ni askari na wamefungua kesi kwamba anaishi na mwanafunzi.


Kamanda huyo amesema lengo lao ilikuwa Haule atoe fedha za hongo au kutoa mahali ambapo inadaiwa hivi karibuni ndugu hao wa mwanamke walikwenda kumchukua ndugu yao na kumrudisha nyumbani.


SomaZaidi:https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/adaiwa-kujinyonga-kisa-wazazi-kumchukua-mpenzi-wake--4495708

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso