TMDA YASHAURIWA KUONGEZA NGUVU YA KUDHIBITI BIDHAA FEKI ZA DAWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 18 August 2023

TMDA YASHAURIWA KUONGEZA NGUVU YA KUDHIBITI BIDHAA FEKI ZA DAWA


Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na UKIMWI Mh. Stanslaus Nyongo akieleza jambo wakati kamati hiyo ikiwa kwenye kikao ilipokutana na Wizara ya Afya kupokea taarifa ya utelelezaji wa majukumbu mbalimbali ya wizara hiyo.
Naibu waziri wa Afya Mh. Dkt. Godwin Mollel (MB) Akifafanua jambo mbele ya kamati ya Kudumu ya Bunge Afya na UKIMWI wakati ilipokutana na wizara hiyo Leo tarehe 17 Agosti 2023 jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Afya na UKIMWI, Mh. Dkt. Faustine Ndungulile akiuliza swali katika kikao cha Kamati kilichofanyika Leo tarehe 17 Agosti 2023, jijini Dodoma.
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba TMDA, Bw. Adam Fimbo, akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma za Afya na UKIMWI tarehe Leo 17 Agosti 2023, jijini Dodoma
Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu, akijibu hoja za wajumbe katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Afya na UKIMWI tarehe leo 17 Agosti 2023, jijini Dodoma.


Na. WAF, Dodoma

Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Stanslaus Nyongo ameitaka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kuongeza nguvu ya kudhibiti bidhaa feki za dawa zinazoingia nchini Tanzania.


Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Nyongo ameyasema hayo  Agosti 17, 2023 baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Bw. Adam Fimbo katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma.


“Tunaona juhudi mnazofanya za kuteketeza dawa feki zinazoingia nchini, hii inaonesha bado kuna mianya mingi ya kuingiza dawa nchini hivyo ni muhimu sana kuongeza nguvu ya kudhibiti uingizwaji wa dawa feki”, amesisitiza Mhe. Nyongo


Aidha, Mhe. Nyongo ameitaka Mamlaka hiyo kuangalia ufanisi wa dawa zilizopo kwa maana kuna baadhi ya dawa hazina ubora mzuri unaotakiwa kulingana na dawa husika hasa kwenye dawa wa ‘Antibiotic’.


“Kuangalia ufanisi wa dawa iwe kipaumbele cha kwanza hasa kwenye hizi dawa za ‘Antibiotic’, maaana anaweza kuja mgonjwa anasema nikitumia dawa hii inaniponyesha kwa haraka kuliko nikitumia dawa hii, Sasa hii ni changamoto kwenu mkalifanyie kazi”, amesema Mhe. Nyongo


Kwa upande wake Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu katika suala la ubora wa dawa amesema linaangaliwa katika mambo Matatu, Kwanza Ubora, Pili usalama na Tatu ufanisi.


“Kwanza tunaangalia swala la ubora, Pili tunaangalia usalama na Tatu tunaangalia ufanisi, kwa hiyo hapa TMDA mnatakiwa kuongeza nguvu kwenye ufanisi wa dawa”, amesema Waziri Ummy


Pia, Waziri Ummy ameipongeza TMDA kwa jitihada wanazofanya kwenye TEHAMA kwa kuwa hakuna malalamiko yeyote ya mtu kukwama usajili kwa muda wa miaka Miwili”, amesema Waziri Ummy


Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Bw. Adam Fimbo amesema, Usajili wa waganga wa tiba asili nchini ulianza Mwaka 2010 ambapo hadi Julai Mwaka 2023, idadi ya wataalam wa Tiba Asili/Mbadala waliosajiliwa ilifikia 47,467 na vituo vya kutolea huduma 1,640 vilikuwa vimesajiliwa.


“Baada ya kufanya usajili huo, matarajio ya Wizara katika kipindi cha mwaka 2023/2024 huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini zitaimarika na kuboreshwa zaidi kwa kuzingatia Sheria na mikakati iliyowekwa na Baraza”, amesema Bw. Fimbo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso