MKUU WA MKOA KILIMANJARO AAGIZA KUKAMILIKA KWA JENGO LA OPD NAIBILI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 18 August 2023

MKUU WA MKOA KILIMANJARO AAGIZA KUKAMILIKA KWA JENGO LA OPD NAIBILI


Mkuu wa Mkoa kilimanjaro Mh. Nurdin Babu ametoa wiki mbili kwa kamati ya ujenzi kuhakikisha wanasimamia hatua za Mwisho (Finishing) kukamilika kwa haraka jengo la wagonjwa wa nje (OPD) Maabara na nyumba ya mtumishi katika zahanati ya Naibili.


Ameyasema ayo akiwa kwenye ziara wilayani Siha Mkoani kilimanjaro akikagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya sita chini Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.


Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha pesa Tsh 271,096,536.00 lengo wananchi wake wapate huduma za Afya kwa Wakati sipo tayari kuona ujenzi huo, kamati ya usimamizi unasuasu hivyo naagiza kituo hicho kijegwe usiku na mchana amesema Nurdin babu Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.

Mbali na hayo yote Mkuu wa Mkoa amewataka kila kiongozi kwa Nafasi Yake katika Almashauri ya wilaya ya Siha kujua kila Mradi unaotekelezwa katika sekta yake kusimamia kwa ukaribu na kuakikisha Mradi unamalizika ukiwa na viwango vya hali ya juu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso