AMUUA MKE NA SHEMEJI YAKE WAKIWA SHAMBANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 18 August 2023

AMUUA MKE NA SHEMEJI YAKE WAKIWA SHAMBANIJESHÄ° la Polisi Mkoa wa Tanga limefanikiwa kumkamata Swalehe Miraji Ally, mwenye umri wa miaka 38 aliyekuwa kakimbilia mkoani Tabora baada ya kufanya mauaji ya mkewe na shemeji yake kwa kuwakata na mapanga mara mbili kichwani wakati wakiwa shambani.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni fundi ujenzi mkazi wa Mkanyageni wilayani Muheza, alimuua mkewe Mwanahawa Hassan (24) na Sauda Sufian (20) kisha kukimbilia Tabora, ambapo jitihada za Polisi zilifanikiwa kumkamata.


Katika tukio linguine polisi imemkamata mkazi wa Handeni, Rajab Athuman mwenye umri wa miaka 32 akituhumiwa kumuua kwa kumkata kichwa kwa kutumia kamba ya katani Helena Sila.


CHANZO:HABARI LEO

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso