HUKUMU YA MFALME ZUMARIDI YAFUTWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 25 August 2023

HUKUMU YA MFALME ZUMARIDI YAFUTWA

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imetengua hukumu ya kifungo cha miezi 12 aliyopewa Diana Bundala maarufu kama "Mfalme Zumaridi" na wenzake wanane baada ya kutiwa hatiani na Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza kwa kosa la kuzuia maofisa wa Serikali kutekeleza majukumu yao.


Uamuzi wa rufaa hizo zilizosajiliwa kwa namba 72/2023 (upande wa mleta maombi, Zumaridi) na namba 32/2023 iliyowasilishwa na upande wa mjibu maombi (Jamhuri) umetolewa leo Ijumaa Agosti, 25 2023, na Jaji Dk Cleoface Morris.


Katika kesi hiyo ya rufaa, upande wa mjibu maombi ulikata rufaa kupinga adhabu hiyo kuwa ndogo kwa mujibu wa sheria, huku upande wa ‘Zumaridi’ nao ukikata rufaa kupinga adhabu hiyo ukidai haikustahili kutolewa.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso