DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 6.1 ZATEKELEZA MRADI WA GHALA LA KUHIFADHIA CHAKULA SUMBAWANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 4 August 2023

DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 6.1 ZATEKELEZA MRADI WA GHALA LA KUHIFADHIA CHAKULA SUMBAWANGA


WAKALA wa Majengo Tanzania TBA, umetekeleza Mradi mkubwa wa ghala la kuhifadhia chakula Tani 21,000 katika Wilaya ya Sumbawanga na umegharimu Dola za kimarekani Milioni 6.1.

Picha ya ghala Sumbawanga

                  
                      NA PAUL KAYANDA-MBEYA


Mradi huo ni wa teknolojia ya kisasa na unatekelezwa katika Mikoa nane ya Tanzania ikiwemo Mikoa ya Nyanda za Juu kusini,Songea, Songwe Makambako, Sumbawanga, Katavi, Shinyanga Manyara na Mkoa wa Dodoma.


Mhandisi wa mradi huo Haruna Kalunga amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari leo Agosti 4, 2023 walipotembelea banda la Wakala wa majengo Tanzania TBA Kwenye sherehe za maonesho ya kimataifa ya kilimo Nane Nane 2023.


Mhandisi Kalunga amebainisha kuwa Miradi wa ghala la kuhifadhia chakula Sumbawanga umeanza kutekelezwa mwezi Januari 2020 na umekamilika mwezi Machi 2023 na umeanza kutumika kwa kuhifadhi mazo ya chakula kwa Wakulima.


"Miradi huo ni wa teknolojia ya kisasa, na unatunza chakula cha walicholima wakulima Tani 21,000 na lengo kuu ni miradi huo kutekelezwa kwa Mikoa 20 lakini kwa sasa tumeanza na Mikoa Nane," alisema Wakala wa majengo Tanzania mhandisi Haruna Kalunga.


Aidha Mhandisi Kalunga alitumia nafasi ya wanahabari hao kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo na kufika katika banda la TBA ili kujua mambo mbalimbali ikiwemo gharama za ujenzi pamoja wa nyumba za makazi na taasisi za serikali kwa gharama nafuu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso