NFRA KUTOA ELIMU KWA WAKULIMA MAONESHO YA KIMATAIFA YA KILIMO NANENANE JIJINI MBEYA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 4 August 2023

NFRA KUTOA ELIMU KWA WAKULIMA MAONESHO YA KIMATAIFA YA KILIMO NANENANE JIJINI MBEYA

 


Kaimu wa wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) kanda ya Songwe, CPA Eva Michaeli Kinavava katika maonesho ya kimataifa ya nanenane yanaoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya amewataka wakulima pamoja na wananchi wengine kufika kwenye banda lao ili wapate elimu ya uhifadhi wa mazao ya chakula na ubora wa utunzaji nafaka.


NA PAUL KANYANDA


Amesema kuwa katika kipindi hiki Wakala huyo wapo katika kipindi cha ununuzi wa nafaka na kuongeza kuwa kama kanda ya Songwe na mkoa wa Mbeya wanaendelea na ununuzi pamoja na mpunga, kwa Mkoa wa Songwe wanavituo vya ununuzi wa mahindi ambavyo Kituo cha Mbozi ofisini,kituo cha Ileje katika soko la Isongole pamoja na Wilaya ya Momba katika maghara ya Halmashauri.


Kaimu Meneja huyo wa NFRA kanda ya Songwe alikuwa akizungumza jana na vyombo mbalimbali vya Habari katika banda lake la NFRA kwenye maonesho ya kimataifa ya kilimo Nanenane 2023 jijini Mbeya.


Alisema kuwa kwa Mkoa wa Mbeya wana kituo kikubwa cha ununuzi wa zao la mahindi na mpunga kituo kipo Kyela na skimu ambazo zipo Ipatagwa pamoja na Mgulumbaya na kwmba huko ndiko ambako wanaendelea na ununuzi wa nafaka.


''Lakini pia ufunguaji wa vituo unaendelea kutokana na upatikanaji wa nafaka eneo husika na bei ambayo tunaitumia ni bei ya soko ,''alisema kaimu Meneja wa wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) kanda ya Songwe, CPA Eva Michaeli Kinavava.


Kauli mbiu kwa mwaka huu, ''Vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu na chakula''

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso