AFUNGWA JELA MIAKA 15, ALIMFANYIA UPASUAJI WA NGIRI MZEE WA MIAKA 78 KWA KUMPASUA TUMBO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 14 August 2023

AFUNGWA JELA MIAKA 15, ALIMFANYIA UPASUAJI WA NGIRI MZEE WA MIAKA 78 KWA KUMPASUA TUMBO


Mahakama kuu kanda yaTabora imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka kumi na Tano jela AMOS MATHIAS mkazi wa Kijiji cha Nhungulu wilayani Nzega baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia kwa kujifanya Daktari na kumfanyia upasuaji wa tumbo na sehemu za siri mzee mwenye umri wa miaka 7
8 ambaye alikuwa na tatizo na ugonjwa wa mshipa wa ngiri.


Akisoma hukumu hiyo Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Tabora, ATHUMAN MATUMA alisema mahakama imepitia hoja za pande zote mbili zilizokubaliana yaani Upande wa Jamhuri na upande wa utetezi, kwamba mshtakiwa ni kweli alitenda mauaji hayo pasipo kukusudia.


Ilieleza mahakamani hapo kwamba mshtakiwa AMOS aliwatoza ndugu wa marehemu kiasi cha shilingi laki mbili kufanya upasuaji huo ambapo walimtangulizia shilingi laki moja na arobaini na alipoona tatizo limekuwa kubwa kwa maana mgonjwa hali ilizidi kuwa mbaya aliwapa maelekezo wamkimbize hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi.


Jaji ATHUMAN MATUMA alitoa adhabu hiyo ya kutumikia kifungo cha miaka 15 ili kukomesha uovu alioutenda AMOS ilihali alikuwa akijua kwamba yeye hana ujuzi wa upasuaji huo uliosababisha kifo cha Mzee Kikongwe.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso