WANAFUNZI WA KITANZANIA WAOMBWA KUPENDA MASOMO YA SAYANSI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 14 August 2023

WANAFUNZI WA KITANZANIA WAOMBWA KUPENDA MASOMO YA SAYANSI



Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Maulilio Kipanyula amewahimiza wanafunzi wa kitanzania kupenda masomo ya sayansi na teknolojia kutokana na mchango wake katika kuleta maendeleo ya nchi.


Prof. Kipanyula amesema Sayansi na Teknolojia imeleta mapinduzi makubwa kitaifa na kimataifa na hasa katika sekta za elimu, habari, biashara na huduma mbali mbali za kijamii.


Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita imeweka kipaumbele katika sekta ya elimu ambapo imewekeza kwa kiwango kikubwa ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa vya kujifunzia na kufundishia hivyo kuwahamasisha wanafunzi kujifunza kwa bidii na kuwa wabunifu.


Alikuwa akizungumza katika hafla fupi ya kugawa majarida 700 yanayofahamika kama OYLA Africa ambayo yametolewa na kampuni ya Baobab Shalom Limited ya jijini Dar es Salaam kufuatia Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) yaliyosainiwa na mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bahati Geuzye na mkurugenzi wa Baobab Shalom Limited Bw. Yev Semikov katika ofisi za TEA jjijini Dodoma tarehe 14 Agosti 2023.


Mkurugenzi mkuu wa TEA, Bahati Geuzye ameshukuru kampuni ya Baobab Shalom Limited kwa kutoa msaada huo wa majarida kupitia Mfuko wa Elimu unaosimamiwa na TEA na kuongeza kuwa TEA iko tayari wakati wote kushirikiana na wadau wa elimu na kuwahakikishia kuwa misaada ya elimu inayopita kwenye Mfuko wa Elimu wa Taifa inasimamiwa kikamilifu na kutumika kama ilivyokusudiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso