WACHANGA MILIONI 26.6 KUJENGA NYUMBA YA MAPADRI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 6 May 2023

WACHANGA MILIONI 26.6 KUJENGA NYUMBA YA MAPADRI

Waumini wa parokia ya Bikira Maria Mama wa Shauri Njema , Mbulu, jimbo Katoliki la Kahama  wamechanga kiasi cha shilingi milioni 26.6 mifuko ya saruji 119 na tofari 500 ili kuwajengea nyumba ya kukaa Mapadri  wanaofanya kazi yao ya utume hapo  waweze kuishi sehemu nzuri.

Padri Joseph Sekere , Paroko wa parokia ya Bikira Maria Mama wa Shauri Jema , Mbulu , Jimbo Katoliki la Kahama akiwa na wageni rasmi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Nyumba mpya ya Mapadri na uzio wa parokia hiyo ambapo kiasi cha shilini milioni 26.6 zilipatikana na saruji mifuko 119 na tofari 500., Picha na Patrick Mabula.

Na  Patrick Mabula , Kahama.

 

Akiongea katika harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba  Alexander  Kazimil  aliyechangia kiasi cha shilingi  milioni 7 alisema  wameamua kuwajengea nyumba ya kuishi mapadri kutokana na  iliyopo kupitwa na wakati  kwa sababau ilijengwa toka mwaka 1921 wakati parokia hiyo ilipofunguliwa.


 Kazimil na familia yake aliyetoa mchango kiasi cha fedha hizo taslimu  aliwashukuru waumini kwa moyo wao wa kuitikia wito wa mpango huo na kuunga mkono  mradi katika kuwajengea nyumba mpya mapadri , pamoja na  uzio wa parokia  ili kulinda eneo hilo ambalo limekuwa likivamiwa na watu.


Paroko wa parokia hiyo Padri  Joseph Sekere amewapongeza waumini kwa moyo wa kuamua kuanza ujenzi wa nyumba mpya ya kukaa  waweze kukaa katika mazingira mazuri kutokana na iliyopo, kuwa ya zamani na ilijengwa  toka mwaka 1921 zaidi ilipofunguliwa na wamisionari wa kizungu waliofika Africa kueneza injili.


 Padri Sekere alisema moyo na ukarimu huo ni kuuitika wito wa Kristu katika moja ya kazi ya Mungu katika kuitegemeza kanisa kwa hali na mali ili watumishi wake waondokane na changamoto ya kukaa katika nyumba ya zamani yenye zaidi  miaka 100 toka kufunguliwa kwa parokia hiyo mwaka 1921.

 

Naye mgeni rasmi katika harambee hiyo Benjamin Ngayiwa  na kusindikizwa na ndugu na jamaa zake ambako  kwa upande wake waliweza kuchangia zaidi ya kiasi cha milioni sita na kuwashukuru  waumini wa parokia hiyo kwa moyo walionyesha wa kujitoka katika kushiriki kazi ya Mungu ili mapadri waweze kukaa sehemu  nzuri wanapowatumikia.

 

Parokia ya Bikira Maria Mama wa Shauri Jema , Mbulu jimbo Katoliki la Kahama ilifunguliwa mwaka 1921 wakati huo ikiwa chini ya Jimbo kuu la Tabora ambapo nyumba ya kuishi mapadri imepitwa na wakati ambapo waumini wameamua kujitoa kujenga nyumba ya kisasa ya kuishi watumishi hao wa Mungu na kuweza kuanza kuchanga kiasi cha sh.26.6 milioni mifuko ya saruji 119 na tofari 500.

 

Mwisho.

Mgeni rasmi katika halambee ya ujenzi wa nyumba ya Mapadri , Meneja wa Raslimali watu wa Benki ya CRDB , Benjamin Ngayiwa akiwa na Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Shauri Jema , Mbulu jimbo la Kahama , Padri Joseph Sekere wakipokea michango katika halambee ya fedha za ujenzi wa nyumba ya mapadri na uzio wa parokia hiyo.Picha na Patrick Mabula.

Mpambe wa mgeni rasmi Alexander Kazimil na mke wake Catherine Alexander wa parokia ya Bikira Maria Mama wa Shauri Jema , Mbulu jimbo la Kahama  wakiongea  baada ya kukabidhi mchango wa familia yake kiasi cha shilingi milioni 7 katika adhimisho la misa ya halambee iliyofanyika katika viwanja vya parokia hiyo katikati ni Paroko wa parokia hiyo Padri Joseph Sekere , Picha na Patrick Mabula.


Mgeni Rami Benjamin Ngayiwa  katika halambee ya ujenzi wa nyumba ya Mapadri na uzio wa parokia ya Bikira Maria Mama wa Shauri Jema , Mbulu , Jimbo la Kahama akiipongeza familia ya Alexander Kazimil na mkewe Catherine kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 7 katika halambee hiyo , Picha na Patrick Mabula.

Mgeni rasmi katika halambee ya ujenzi wa nyumba ya Mapadri na uzio wa parokia ya Bikira Maria Mama wa Shauri Jema , Mbulu , Jimbo la Kahama  , Benjamin  Ngayiwa alipokuwa akitangaza kiasi cha fedha zilizopatikana  jumla ya shilingi 26.6 milioni , mifuko ya saruji 119 na tofari 500  , Picha na Patrick Mabula.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso