MWANAFUNZI DARASA LA SABA BULIGE "A" HALMASHAURI YA MSALALA AFUKUZWA SHULE KWA TUHUMA ZA WIZI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 2 May 2023

MWANAFUNZI DARASA LA SABA BULIGE "A" HALMASHAURI YA MSALALA AFUKUZWA SHULE KWA TUHUMA ZA WIZI

Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Bulige “A” Emmanuel George katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga amemfukuza shule mwanafunzi wa Darasa la saba kwa tuhuma za kuiba Nondo (pisi) za madirisha ya madarasa ya shule.



Akizungumzia tukio hilo baba mzazi wa mtoto huyo aliefukuzwa shule mwenye umri wa miaka 15 jina limehifadhiwa Emmanuel John amesema mnamo March 25, 2023 alipigiwa simu, mwanae amekamatwa na Nondo za madirisha mali ya shule ya msingi Bulige “A”.


Amesema baada ya kufika shuleni alikuta mwanae amekabidhiwa kwa jeshi la sungusungu ambapo alitakiwa kulipa faini ya shilingi laki sita na Elfu hamsini (650,000) kama faini ambapo laki moja na Elfu hamsini kwa ajili ya jeshi la sungusungu na shilingi laki tano kwa ajili ya Shule.


Mzazi Emmanuel John baada ya kuhoji kuhusu mwanae kupelekwa sungusungu jambo ambalo ni hatari kwa mwanae kwani yeye alihitaji angekabidhiwa kwenye kamati ya shule lakini jambo hilo halikufanyika.


Baada ya siku mbili aliitwa shuleni kwenye kamati ya shule na kupewa taarifa kuwa mwanae amefukuzwa shule na ndani ya siku kumi na nne (14) atakabidhiwa barua ya mtoto kufukuzwa shule.


“Niliitwa shuleni nilipofika niliwakuta kamati ya shule wakanisubirisha nje baadae wakaniita na mwalimu mkuu akaanza kuniambia mtoto amefukuzwa shule, nikawaambia kamati huyu ni mtoto alipaswa kuonywa tu kwa adhabu akaendelea na shule”.


“Kesho yake nikaenda kwa diwani akaniambia mtoto mwambie aende shule wakimfukuza nitampigia simu wamemfukuza, ilivyofika April 21, 2023 mwanangu alienda kufanya mitihani ya kujipima alifukuzwa kwa kukimbizwa na mwalimu mkuu na barua ikaletwa ya kufukuzwa”.


“Mimi kama mzazi ninaomba nisaidiwe mtoto wangu amalizie shule sehemu ambayo inasemwa ameharibu nitatengeneza lakini mwalimu mkuu hataki kabisa sijajua huyu mwalimu ana shida gani na mwanangu”.


Kwa upande wake mwalimu mkuu wa Bulige “A” Emmanuel George amesema yeye sio msemaji wa jambo hilo bali aulizwe mwajiri wake ambaye hakumtaja jina huku akisema taarifa hizo sio za kupelekwa kwa wandishi wa habari hivyo waulize hao hao waliotoa taarifa hizo.


Aidha kwa mujibu wa barua ya kufukuzwa shule kwa mwanafunzi huyo ambayo imesainiwa na mwalimu mkuu huyo imesema mwanafunzi amefukuzwa kuanzia April 20, 2023 na hatakiwi kufika eneo la shule na atakapoonekana atakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama kama mhalifu.





No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso