MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIEDAIWA KUMUUA JIRANI YAKE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 24 February 2023

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU ALIEDAIWA KUMUUA JIRANI YAKE


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemwachia huru, dereva Boi Rajabu (65) aliyekuwa aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya mauaji, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.


Rajabu anadaiwa kumuua jirani yake aitwaye, Abbas Mwinjuma kwa kumchoma kisu tumboni hadi utumbo ukatoka nje, tukio analodaiwa kulifanya Februari 8, 2019 katika eneo la Mbweni Miti mitatu, Wilaya ya Kinondoni.


Hukumu hiyo imetolewa jana Alhamisi, Februari 23, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu Romuli Mbuya, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.


"Hakuna ushahidi wowote wa upande wa mashtaka ulionyesha kuwa Rajabu alimuua Abbas na hata mashahidi sita wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi wao hapa mahakamani wamehadithiwa na Adam Matutu, ambaye upande wa mashtaka walitakiwa kumleta mahakamani ili aje atoe ushahidi, lakini kwa bahati mbaya sana hawakumleta.


"Tukio limetokea uani katika nyumba ambayo Abbas anaishi na mama yake na kutoka katika nyumba ya mtuhumiwa hadi hapo uani kwa kina Abbas ni umbali wa mita sita, kwa nini hakuna jirani yoyote wa eneo hilo aliyeenda kugonga mlago wa Boi kujua yupo au hayupo ili wamkamate?


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso