AUA MKE, MTOTO MCHANGA KWA KISU KISA WIVU WA MAPENZI- KILIMANJARO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 24 February 2023

AUA MKE, MTOTO MCHANGA KWA KISU KISA WIVU WA MAPENZI- KILIMANJARO

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwanaume mmoja, mkazi wa Mero, wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro kwa madai ya kumuua mkewe na kumjeruhi mtoto mchanga kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.


Mwanamke huyo ambaye anatambulika kwa jina la Fausta Tesha (26) aliuawa kwa kukatwa na kisu sehemu za tumboni, kifuani na ubavuni pamoja na kichanga chake usiku wa kumkia jana, Februari 23, mwaka huu.


Kwa mujibu wa Polisi, mtoto huo mchanga wa wiki mbili amelazwa katika hospitali ya KCMC kwa ajili ya matibabu baada ya kuchomwa kisu tumboni na kusababisha utumbo kutoka nje.


Akizungumza na Mwananchi digital jana Februari 23, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Simoni Maigwa amesema wanamshikilia mwanaume huyo kutokana na mauaji ya mke wake.


"Mwanaume huyu amemuua mke wake na kumjeruhi mtoto wa wiki mbili kwa wivu wa mapenzi, huyu mwanaume alienda kwenye machimbo huyu mwanamke akawa amepata ujauzito, sasa ikaonekana kuna mgogoro wa familia juu ya huyu mtoto," amesema.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso