UPELELEZI WA KESI YA DAWA ZA KULEVYA INAYOMKABILI KOCHA WA SIMBA NA WENZAKE WAKAMILIKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 2 January 2023

UPELELEZI WA KESI YA DAWA ZA KULEVYA INAYOMKABILI KOCHA WA SIMBA NA WENZAKE WAKAMILIKA

Upelelezi wa kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine kilo 34.89 inayomkabili aliyekuwa kocha wa makipa wa timu ya Simba Sport Club, Muharami Sultan (40) na wenzake watano, umekamilika.


Tayari Serikali imeshapeleka nyaraka muhimu za kesi hiyo Mahakama Kuu kwa ajili ya kusajiliwa na kisha washtakiwa hao watasomewa maelezo ya mashahidi na vielelezo kabla ya kuhamishwa Mahakama ya juu.


Wakili wa Serikali, Caroline Matemu ameieleza Mahakama ya Hakimu ya Hakimu Mkazi, leo Januari 2, 2023, wakati kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 71/2022 ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.


Matemu ametoa maelezo hayo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.


Sultani na wenzake, wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo 34.89.


Wakili Matemu amedai upelelezi wa shauri hilo umekamilika, hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuja kuwasomewa washtakiwa idadi ya mashahidi na vielelezo.


Hakimu Mrio, baada ya kusikiliza maelezo ya upande wa mashtaka, ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 16, 2023 itakapotajwa na washtakiwa wapo rumande kutokana na kesi inayowakabili haina dhamana kwa mujibu wa sheria.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso