MIKUTANO YA HADHARA SASA YARUHUSIWA RAIS SAMIA AVITAKA VYAMA VYA SIASA KUHESHIMU SHERIA ZA NCHI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 3 January 2023

MIKUTANO YA HADHARA SASA YARUHUSIWA RAIS SAMIA AVITAKA VYAMA VYA SIASA KUHESHIMU SHERIA ZA NCHI


Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameruhusu mikutano ya hadhara iiliyokuwa ikililiwa kwa muda mrefu na vyama vya upinzani kutaka ruhusiwe.


Leo Jumanne, Januari 3, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Samia amesema; "uwepo wangu leo hapa mahali nimekuja kufanya ruhusa ya mikutano hii, nimekuja kutangaza kuondoa zuio la kuzuia mikutano ya hadhara na ninasema kwamba, sasa linaondoka."


Rais Samia amesema mikutano hiyo kisheria, ni haki haki kwa vyama vya siasa kuiendesha huku akisema kwa upande wa Serikali wamejipanga kutekeleza wajibu wao wa kulinda mikutano hiyo.


Ili kuendelea na mikutano hiyo, Rais Samia amesema jukumu sasa linabaki kwa vyama vya siasa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola kama sheria na kanuni zinavyoelekeza ili vipatiwe ulinzi.


Rais amesema hatua waliyoifikia katika mazungumzo baina ya vyama hivyo na Serikali kwa sasa, mikutano hiyo haitazuiliwa tena.


"Ruhusa ya mikutano ya kisiasa itatolewa, wajibu wetu sisi Serikali ni kuwalinda mfanye mikutano yenu salama mmalize vizuri, kufuata kanuni ndio wajibu wenu vyama vya siasa," amesema.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso