MWANAUME MMOJA AKUTWA AMEFARIKI CHUMBANI KWAKWE HUKU MZIKI UKILIA,SHINYANGA. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 3 January 2023

MWANAUME MMOJA AKUTWA AMEFARIKI CHUMBANI KWAKWE HUKU MZIKI UKILIA,SHINYANGA.


Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 32 Mkazi wa Kambarage Manispaa ya Shinyanga, Daud John amekutwa akiwa amefariki chumbani kwake.

Wananchi wa Kambarage Mkoani Shinyanga waliofika eneo la tukio.

NA HALIMA KHOYA,SHINYANGA.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Januari 2,2023 ambapo marehemu Daud John alikuwa ni mmoja wa wapangaji wa Nyumba ya Mzee Hangwa katika mtaa wa Kambarage kata ya Kambarage katika Manispaa hiyo Mkoani Shinyanga.


Huheso Digital imefika katika eneo la tukio na kuzungumza na Mwenyekiti wa mtaa wa Kambarage Bwana Malick Juma Mbasha ambaye ameeleza kuwa amepokea taarifa hizo leo asubuhi na baada ya kufikia kwenye familia hiyo alipiga simu kituo cha polisi kutoa taarifa.


“Nilikuwa ofisini kwangu asubuhi alikuja balozi wa nyumba kumi akasema kwenye nyumba ya mzee Hangwa kuna kijana amekutwa amefariki basi tumefika kwenye tukio tukaambiwa huyu kijana mara ya mwisho alionekana siku ya jana na alikuwa ndani analiza mziki lakini asubuhi ya leo tumemkuta amefariki na mziki ukiendelea”.amesema Mwenyekiti Malick Mbasha


Aidha Mwenyekiti huyo amewataka wananchi wa mtaa huo ambao hawafahamiki kwenye ofisi ya serikali ya mtaa kupeleka taarifa zao sahihi ili kuepusha changamoto pale zinapotokea.


Nao baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo wakiwemo wapangaji katika nyumba hiyo wamesema marehemu huyo hakuwa na tatizo lolote la kiafya ambapo baada ya kugundua kifo chake walikuta amefariki akiwa amelala kitandani huku mziki ukiendelea kulia chumbani kwake.


Aidha kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi ambaye amedhibitisha kifo cha Daud John.


Kamanda Magomi amesema jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linaendelea na upelelezi ili kubaini chanzo cha kifo.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso