NAFASI 9 ZA KAZI - DEBRA MICROFINANCE KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 3 January 2023

NAFASI 9 ZA KAZI - DEBRA MICROFINANCE KAHAMADEGRA FINANCE SERVICES COMPANY LIMITED (DFSCL) iliyopo wilayani Kahama - Mkoani Shinyanga ni kampuni inayojihusisha na utoaji wa mikopo kwa wajasiliamali wadogo wadogo wenye mitaji ya Tsh.50,000 hadi Tsh.5,000,000.

Degra Finance Services Company Limited inapenda kutangaza nafasi mpya za kazi kwa wale wenye sifa kama ifuatavyo:

AFISA MIKOPO (CREDIT OFFICER) – NAFASI NNE(4)

Sifaza Muombaji:

i. Muombaji awe mtanzania

ii. Awe na Umri kuanzia miaka 18 – 30

iii. Awe ana elimu kuanzia ngazi ya Astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma) katika kada za Biashara, Fedha, Benki, Uhasibu na masoko

iv. Uwezo mzuri wa kufanya kazi kwa ushirikiano (Teamwork)

v.Uwezo mzuri katika stadi za mawasiliano (Communication Skills)
vi. Awe na uwezo wa kutumia kompyuta

vii. Awe tayari kufanya kazi mahali popote


MKUSANYA MADENI (DEBT COLLECTOR)-NAFASI NNE(4)

Sifa za Muombaji:

i. Muombaji awe mtanzania

ii. Awe na Umri kuanzia miaka 18 – 30

iii. Awe ana elimu kuanzia ngazi ya Astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma) ya Biashara/Utawala/Masoko/uhasibu/sheria

iv. Uwezo mzuri wa kufanya kazi kwa ushirikiano (Team work)

v. Uwezo mzuri katika stadi za mawasiliano (Communication Skills)


SECRETIRIAL NAFASI MOJA(1)

i. Awe na astashahada ya kopyuta

Jinsi ya kutuma Maombi ya Kazi:

Tuma barua ya maombi na Wasifu (CV) kupitia  email yetu  ya degrafinanceltd@gmail.com

Au wasilisha katika ofisi zetu zilizopo barabara ya Tabora kata ya nyihogo karibu na Losha hotel.


Mwisho wa Kutuma Maombi: Tarehe  17/01/2023

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso