MKUU WA MKOA SHINYANGA SOPHIA MJEMA ATEULIWA KUWA KATIBU MWENEZI WA CCM. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 14 January 2023

MKUU WA MKOA SHINYANGA SOPHIA MJEMA ATEULIWA KUWA KATIBU MWENEZI WA CCM.

Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi " CCM" Taifa, imefanya mabadiriko madogo ya Wajumbe wa Sekretarieti, huku Sophia Edward Mjema ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ikimteua kuwa Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Taifa.

Na Juma Mwesigwa, Huheso Digital Kahama.


Mjema anachukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Shaka Hamidu Shaka,huku aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama kwa awamu iliyopita,Anamringi Macha, akiteuliwa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara.


Katika Kikao hicho Maalum cha kwanza cha Halmashauri Kuu ya  CCM Taifa kwa Mwaka 2023 kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Januari, 2023,kimeendelea kumkasimisha nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama hicho   Daniel Chongolo. 

Ndugu Sophia Mjema
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalum cha kwanza cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Taifa kwa Mwaka 2023 

Wajumbe wengine wa Sekretarieti ya CCM Taifa walioteuliwa ni pamoja na:-


Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
Said Mohamed Dimwa


Dkt. Frank Haule
Katibu wa Uchumi na Fedha


Mbarouk Nassor Mbarouk
Mkuu wa Idara ya Kimataifa


Issa Haji Gavu
Idara ya Organaizeisheni

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso