MAKAMU WA RAIS PHILIP MPANGO KUFANYA ZIARA MKOANI SHINYANGA KUANZIA KESHO JUMATANO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 17 January 2023

MAKAMU WA RAIS PHILIP MPANGO KUFANYA ZIARA MKOANI SHINYANGA KUANZIA KESHO JUMATANO


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo Jumanne Januari 17,2023 kwenye Hospitali mpya ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo Jumanne Januari 17,2023 kwenye Hospitali mpya ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango anatarajiwa kufanya ziara Mkoani Shinyanga ambapo miongoni mwa shughuli atakazofanya ni pamoja na kuweka Jiwe la Msingi Hospitali ya Mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo katika kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumanne Januari 17,2023 akiwa kwenye Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda amesema uwekaji wa jiwe la msingi katika hospitali hiyo inayoendelea kujengwa utafanyika kesho Jumatano Januari 18,2023.


“Akiwa mkoani Shinyanga Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ambapo atawasili leo mkoani Shinyanga na kesho atakuwa Isaka wilayani Kahama kwa ajili ya kuzindua Ujenzi wa kipande cha nne cha Reli ya Kisasa (SGR) cha Isaka – Tabora lakini pia atakuja kuweka jiwe la msingi katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na Januari 19,2023 atafungua mradi mkubwa wa maji wa Tinde – Shelui”,amesema Dkt. Mawanda.


Dkt. Nawanda ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amewaomba wakazi wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kumpokea Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso