MITI ELFU MOJA YAPANDWA NA JESHI LA POLISI, SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 14 January 2023

MITI ELFU MOJA YAPANDWA NA JESHI LA POLISI, SHINYANGA

Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga kushirikiana na wadau mbalimbali limeendesha zoezi la upandaji miti ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono agizo la makamu wa Rais la kuhakikisha kila halmashauri inapanda miti Million 1 na laki 5 ili kuendana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga,ACP,Janeth Magomi akiwa anapanda mti ili kuendana na mabadiliko ya tabia ya nchi

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akipanda mti Manispaa ya shinyanga



NA HALIMA KHOYA, HUHESO DIGITAL SHINYANGA.


Zoezi hilo limefanyika leo januari 13,2023 ambapo miti 200 imepandwa katika kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) na miti 800 imepandwa katika eneo la hospitali ya Rufaa mkoani humo.


Akieleza lengo la kuendesha zoezi hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga,ACP,Janeth Magomi,Amesema kuwa wameamua kupanda miti elfu 1 ikiwa ni sehemu ya kutunza mazingira sambamba na kuendana na mabadiliko ya hali ya hewa.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,jasinta Mboneko,Amelipongeza jeshi la Polisi kwa kuunga mkono juhudi za upandaji miti katika Wilaya hiyo sambamba na kuwasisitiza wananchi kuendeleza kupanda miti ya kimvuli na matunda kwaajili ya kutoa fursa mbalimbali za kibiashara pamoja na lishe ya watoto na watu kwa ujumla.


“Awali kampeni hiyo ilizinduliwa mwaka jana,na mwaka huu imeendelezwa na jeshi hili hivyo tutaendelea kupanda miti ili shinyanga yetu iendelee kuwa ya kijani,nawasisitiza wananchi ni marufuku kukata miti bila kibali na wale wanaomiliki mifugo hamtakiwi kupitisha katika maeneo ya Manispaa kwasababu inachqafua mazingira na kula miti yetu”Amesema Mboneko.


Aidha Kwa upande wake Afisa maliasili Manispaa ya Shinyanga,Ezra Manjerenga,amesema licha ya kupata faida ya kuendana na tabia ya nchi pia upandaji wa miti ya matunda unasaidia kuweka usawa wa lishe katika jamii.


”ukipanda mti wa matunda katika kaya yako,tofauti na kupata faida ya hali ya hewa lakini pia unapata faida ya kuipatia familia yako lishe,tunahamasisha mpande miti ya matunda michache ambayo ni imara ”Amesema Manjerenga.


Nae mgaga mkuu wa hospitali hiyo Dkt .Luzira John ameahidi kusimamia utuzaji wa miti hiyo iliyo padwa katika hospitali kwa kuweka watu wakuituza na kuimwagilia wakati wa kiangazi hali itakayo saidia kupendezesha mazingira ya hospitali hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso