WIVU WA MAPENZI WASABABISHA KIFO CHA MWANAMKE ,SHINYANGA. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 14 January 2023

WIVU WA MAPENZI WASABABISHA KIFO CHA MWANAMKE ,SHINYANGA.

Joyce masanja (30-35) Mkazi wa Mtaa wa kalonga Manispaa ya Shinyanga anasadikiwa kuuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali na mtu asiyefahamika katika mbali mbali za mwili wake hali iliyopelekea kifo chake.

Wananchi waliofika Eneo la tukio kushuhudia mauaji hayo Mtaa wa Kalonga Manispaa ya Shinyanga 

Mtaa wa Kalonga Manispaa ya Shinyanga, kwenye tukio hilo


NA HALIMA KHOYA, Huheso Digital SHINYANGA.


Tukio hilo la mauaji limetokea usiku wa kuamkia leo january 14,2023 majira ya saa 6 katika mtaa wa kalonga Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Mkoani humo.


Akieleza juu tukio hilo jirani wa marehemu huyo,Rose Galani,amesema majira ya saa sita usiku alisikia kelele na vishindo vikubwa kwenye dirisha lake ambapo aliamka na kuchungulia ndipo alipokuta wanaume wawili na mwanamke mmoja wakiwa wanapita.


”Ilikuwa mida ya saa 6 hivi nikasikia kelele kwa dirishani nikawa nimechungulia nikakuta wanaume wawili na mwanamke mmoja nikajua wanapita tu,sasa asubuhi ndipo nilipoambiwa kuna mwanamke ameuliwa usiku ndo nikastuka kumbe ndo kelele zile nilizokuwa nasikia,tunaiomba serikali iweke ulinzi shirikishi maana matukio yanayotokea ni makubwa”Amesema Rose Galani.


Kwa upande wake kaka wa marehemu,Ezekiel james,amesema alipigiwa simu na kuambiwa kuwa dada yake ameuliwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali na kwamba alipoulizia chanzo cha kufanyiwa ukatili huo aliambiwa siku chache kabla familia hiyo ilikuwa na ugomvi ambapo mume alikuwa anataka kuuza nyumba na mke akawa anakataa.


Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo,Victor Ochieng,Amesema kuwa amepata taaifa za tukio hilo majira ya saa 12 asubuhi ambapo aliafika eneo la tukio na kukuta ni kweli mauaji hayo yamefanyika na kwamba alitoa taarifa Polisi kwaajili ya uchunguzi Zaidi.


Victor,ametoa wito kwa wananchi wa mtaa huo kufika katika uongozi kwaajili ya kupeleka malalamiko yao ili kuondokana na vitendo vya kikatili katika jamii na kuacha kujichukulia sheria mkononi.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga,ACP,Janeth Magomi,amethibitisha tukio hilo kwa kusema kuwa Jeshi hilo tayari linamshikilia Mtuhumiwa ambaye ni mume wa marehemu kwa kuwa inaelezwa kabla ya tukio mwanaume alimtuhumu mkewe kutoka kimapenzi na mwanaume mwingine.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso