KIJANA WA MIAKA 19 APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUMWINGILIA KINYUME NA MAUMBILE MTOTO WA MIAKA NANE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 19 January 2023

KIJANA WA MIAKA 19 APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUMWINGILIA KINYUME NA MAUMBILE MTOTO WA MIAKA NANE

Mkazi wa eneo la Ilkiding'a wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha, Calvin Abraham (19) amepandishwa kizimbani akikabiliwa na makosa mawili ya ulawiti na ubakaji wa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka nane.


Leo Alhamisi Januari 19, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Bittony Mwakisu mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Agosti hadi Septemba 5, 2022.


Akimsomea mashtaka hayo, Wakili wa Serikali, Neema Mbwana alidai kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni mfanyakazi wa hoteli, ametenda makosa hayo kinyume na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.


Alidai kosa la kwanza ni kulawiti kinyume na kifungu cha 154(1) a na 2, cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.


Alisema kuwa mtuhumiwa huyo anadaiwa kufanya kosa hilo eneo la Ilboru ya Juu, kwa kumwingilia kinyume na maumbile mwanafunzi mwenye umri wa miaka nane.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso