MAKAMU WA RAISI DKT.PHILIP MPANGO ATOA AGIZO WEZI WA MAJI WAKAMATWE,IKIWEZEKANA WAJENGE VISIMA VYAO,SHINYANGA. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 20 January 2023

MAKAMU WA RAISI DKT.PHILIP MPANGO ATOA AGIZO WEZI WA MAJI WAKAMATWE,IKIWEZEKANA WAJENGE VISIMA VYAO,SHINYANGA.


Makamu wa Raisi Dkt.Philip Mpango,Ametoa agizo kwa kamati ya ulinzi na usalama,Wizara na vyombo vya Dola kuwakamata wabadhilifu na wezi wa maji ya ziwa viktoria pamoja na wale wanaochepua maji na kuyawekea uzio kuacha mara moja ili kunufaika na fedha zinazotolewa na Raisi Mhe,Samia Suluhu Hassan ili kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo.

Makamu wa Raisi Dkt.Philip Mpango akiwa katika zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi wa maji kutoka ziwa viktoria kwendaTinde-Sherui.


Viongozi wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika hafla ya uwekwaji wa jiwe la msingi mradi wa maji.

Makamu wa Raisi Dkt.Philip Mpango akishiriki zoezi la upandaji wa miti katika mradi wa maji.



NA HALIMA KHOYA, Huheso Digital SHINYANGA.


Akitoa hotua leo Januari 19,2023 katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi wa maji kutoka ziwa viktoria kwenda mji wa Tinde na kutoa agizo hilo Mkoani Shinyanga.


Makamu wa Raisi Dkt.Philip Mpango,amesema wabadhilifu hao ni miongoni mwa wawekezaji wakuwba ambao wanahujumu fedha katika mradi huo sambamba na kuchepusha maji kutoka katika ziwa viktoria ambapo wanawekea uzio kwenye maji hayo hali inayowakwamisha wananchi wengine kuyapata huduma hiyo.


Aidha Mpango,Amewataka wananchi na wakazi wa Mkoa wa shinyanga kupanda miti ya aina yote(matunda na kimvuli) ili kunusuru nchi ya Tanzania ambayo imeathiriwa na ukataji miti sambamba na kuweka usawa wa lishe na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.


“Kuna wizi wa maji katika Ziwa Viktoria na wanaobia ni wawekezaji wakuwba,ninawaonya wote mnaojihusisha na ubadhilifu huu,na ninatoa agizo kwa kamati ya ulinzi na usalama,wizara na vyombo vya dola kuwakamata wanaoiba maji,kumekuwa na baadhi ya watu wanaochepua maji kutoka ziwa viktoria na kuweka ukingo ili wengine wasitumie ni marufuku,waangalie uwezekano wa kujenga visima vyao,kwasababu kila binadamu wanahitaji maji na siyo wao peke yao”Amesema Mpango.


Kwa upande wake Waziri wa maji,ambaye ni mbunge wa jimbo la Pangani,Jumaa Aweso,Amesema miaka ya nyuma wizara ya maji ilikuwa wizara ya kero na lawama kwasababu fedha zilikuwa zinatolewa ila matokea hayaonekani ambapo kwa sasa watumishi wa maji wamebadilika na kuwa watumishi wazuri na wenye kutekeleza maagizo ya serikali.


Aweso,amesema kuwa kwa kushirikiana na serikali ya India katika mradi huu wamepewa zaidi bil.600 kwaajili ya kutoa maji kutoka ziwa viktoria na kusambaza katika mikoa ya karibu(Tabora,Igunga na Nzega) na kuhakikisha zaidi vijiji 100 vinapata huduma ya maji ambapo kwa usimamizi mzuri baada ya kuukamilisha mradi ule walibakisha bil.24.4 ambazo zimetumika kukamilisha ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita Mil.1laki 1 na elfu 50.


“wananchi Zaidi ya elfu 60 wanaenda kupata huduma ya maji,Mhe,makamu wa Raisi naomba nikuhakikishie kuwa tunaomba miezi mitatu wakazi wa Tinde ambao wapo kwenye mpango wa kupata maji vijiji 22 watakua wamefikiwa,na ifikapo 2025 upatikanaji wa maji vijijini itafika asilimia 85 na mjini asilimia 95”Amesema Aweso.


Aidha kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Solwa,Ahmed Salum,Amesema anaishukuru serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Samia kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi na uboreshaji wa wizara mbali mbali na kwamba jimbo lake limefanikiwa kukamilisha miradi hiyo kikamilifu.


Salum,amesema kuwa katika jimbo lake maji yatapatikana mara baada ya kukamilika kwa mradi wa maji kutoka ziwa Viktoria huku akiiomba serikali kuwajengea kituo cha afya wakazi wa jimbo lake ili kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso