MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AKUTWA AMEKUFA NDANI KWAKE DAR ES SALAAM - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 20 January 2023

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AKUTWA AMEKUFA NDANI KWAKE DAR ES SALAAM


MWALIMU Gephason Shita wa Shule ya Msingi Tuwapende Watoto, iliyopo Bunju B, Kata ya Mabwepande jijini Dar es Salaam, emekutwa amekufa chumbani kwake katika nyumba aliyokuwa anaishi eneo la Bunju B.


Akizungumza leo wakati wa kuaga mwili wa Gephason katika shule aliyokuwa anafundisha, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Immaculate Mleke, amesema Gephason alifundisha vipindi vya Jumatatu wiki hii, lakini baada ya siku hiyo hakuonekana tena, mpaka walipomtafuta nyumbani kwake na kukuta amefariki.


Amesema Mwalimu huyo aliyekuwa na umri wa miaka 29, akifundisha somo la Hisabati, anasafirishwa kuelekea kijijini kwao Kinazi mkoani Kigoma.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso