AUA MAMA MKWE, MKE WAKE, WATOTO WAKE WATANO NA YEYE KUJIUA KISA TALAKA YA MKE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 6 January 2023

AUA MAMA MKWE, MKE WAKE, WATOTO WAKE WATANO NA YEYE KUJIUA KISA TALAKA YA MKE

Michael Haight mwenye umri wa miaka 42 nchini Marekani amemuua mke wake, mama mkwe na watoto wake 5 na yeye kujiua baada ya mke wake kuwasilisha ombi la talaka jambo ambalo yeye hakulitaka.


Tukio hilo limetokea katika jimbo la Utah nchini Marekani ambapo miili ya watu hao imepatikana ndani ya nyumba ya mashambani katika Jiji la Enoch wakati wa ukaguzi katika boma lao.


Waliofariki ni mke wake Tausha mwenye umri wa miaka 40, mama mkwe wake Gail Earl mwenye umri wa miaka 78 na watoto wake watano pamoja na mhusika huyo Michael Haight.


Polisi wamesema chanzo cha mauaji hayo ni mwanaume huyo kutofurahishwa na ombi la talaka lililowasilishwa na mke wake Desemba 21/2022.


CHANZO:LANGOLAHABARI

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso