MTOTO APIGWA RADI AKICHUNGA MBUZI NJOMBE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 20 December 2022

MTOTO APIGWA RADI AKICHUNGA MBUZI NJOMBE

Calista Haule (15) mkazi wa kijiji cha Lifua kata ya Luilo wilayani Ludewa mkoani Njombe amefariki baada ya kupigwa na radi wakati akiwafunga mbuzi chini ya mti baada ya kuwatoa malishoni


Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema binti huyo alipigwa na radi hiyo na kufa papo hapo sambamba na mbuzi aliokuwa akiwafunga


Baba wa binti huyo pamoja na dada yake wameelezea masikitiko yao na kudai kuwa binti huyo alirejea nyumbani wiki moja iliyopita akitokea shuleni Mafinga mkoani Iringa kwa ajili ya likizo baada ya shule kufungwa.

CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso