NAPE AAHIDI WIZARA YAKE KUZUNGUMZA NA MAHAKAMA KUHUSU MAKOSA YA KIMTANDAO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 19 December 2022

NAPE AAHIDI WIZARA YAKE KUZUNGUMZA NA MAHAKAMA KUHUSU MAKOSA YA KIMTANDAO


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amesema mfumo wa uhakiki, utunzaji wa kumbumbuku za makosa ya mtandao utasaidia kuharakisha upelelezi wa makosa ya mtandao na kupunguza muda wa kuyashughulikia.


Nape ambaye ni Mbunge wa Mtama mkoani Lindi, amesema mfumo huo utasaidia pia kuharakisha upatikanaji wa ushahidi wa makosa ya mtandao.


Waziri huyo, ameeleza hayo leo wakati wa akigawa vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), vilivyotolewa na wizara yake kwenda kwa Jeshi la Polisi na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) kwa ajili ya kutumika kwenye moduli ya makosa ya mtandao.


Nape amesema kumekuwapo na changamoto za takwimu zinazohusu makosa ya mtandaoni baina ya taasisi na wadau, hatua inayosababisha ugumu wa kupata uhalisia wa mwendelezo wa matukio tangu kupokelewa kwa taarifa, kushughulikiwa na namna yanavyoendelea kufanyiwa kazi.


"Kukamilika kwa moduli hii kutatua changamoto kwa taasisi zote zinazoshughulika na makosa ya mtandao ambapo zitakuwa zikitumia mfumo mmoja badala ya mifumo tofauti iliyokuwapo.


"Suala hilo litaharakisha upelelezi wa makosa ya mtandao na kupunguza muda wa kuyashughulikia, ukiangalia mwenendo wa makosa ya mtandaoni sio makubwa lakini yana ongezeka lazima tuchukue hatua ya kuyadhibiti," amesema Nape.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso