BASI LA HAPPY NATION LATEKETEA KWA MOTO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 19 December 2022

BASI LA HAPPY NATION LATEKETEA KWA MOTO


Zaidi ya abiria 50 waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Happy Nation wamenusurika kifo baada ya basi hilo kuteketea kwa moto mkoani Pwani.


Tukio hilo limetokea leo Jumatatu Desemba 19, 2022 saa nne asubuhi maeneo ya bonde la Wami wakati basi hilo likitokea Dar es Salaam kuelekea Arusha.


Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Issa Inkya ameliambia Mwananchi kwamba licha ya basi kutekekea kwa moto hakuna madhara kwa binadamu na wote walitoka salama pamoja na mali zao.


“Kwa mujibu wa maelezo ya watu wangu wameniambia chanzo cha basi kuungua ni hitilafu ya waya katika mfumo mzima wa gari, nipo njiani kuelekea huko kwa jinsi lilivyoungua sidhani kama litafaa kwa matumizi,” amesema Inkya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso