APIGWA RISASI NA WATU WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI,SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 20 December 2022

APIGWA RISASI NA WATU WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI,SHINYANGA


Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 32,Mkazi wa Butengwa Maanispaa na Mkoa Shinyanga,Richald Nzumbe,Amefariki dunia baada ya kuvamiwa na majambazi wawili wanaotumia silaha kisha kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili (kifuani,bega la mkono wa kushoto na kulia, na paja la mguu wa kushoto)hali iliyopelekea kifo chake.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga, ACP, Janeth Magomi


NA HALIMA KHOYA, Huheso Digital SHINYANGA.


Tukio hilo la uvamizi kwa kutumia silaha uliosababisha kifo cha Richald Nzumbe,limetokea Desemba 19,2022 majira ya saa 1 usiku katika Kata ya Butengwa Manispaa ya Shinyanga Mkoani humo.


Akieleza juu ya tukio hilo Mwenyekiti wa Mtaa Butengwa,Onesmo Mayeba,Amesema majira ya saa 1 usiku alipewa taarifa na mwananchi juu ya tukio hilo ambapo alifika eneo husika na kukuta majambazi hao wamekwisha tenda uvamizi huo huku ikisemekana lengo la kufanya uvamizi huo ni kuwania fedha kutoka kwa marehemu Richald.


“Tukio hili ni lakikatili na tunalilaani kwa sababu majambazi hawa wametoa uhai wa mtu ambapo ni kosa la jinai,hivyo tunaliomba jeshi la polisi kuwabainisha wote waliohusika kutenda mauaji hayo na kuwapa adhabu kulingana na Sheria”Amesema Mayenda.


Awali akieleza undani wa tukio hilo Shemeji wa marehemu,Salome Dady, amesema majira ya saa 1 usiku walikuwa ndani yeye na watoto wa dada yake,ndipo waliposikia gari la shemeji yake likiwa limefika getini ambapo mtoto wake alienda kufungua geti hilo ndipo aliposukumwa na majambazi hao na kumfuata marehemu kisha kumfanyia unyama huo.


"Tulikuwa ndani mimi na watoto wa dada mara tukasikia gari likiwa getini ambapo alienda mtoto wa dada kufungua mlango ndipo nikasikia kelele nje ikabidi nitoke nikaone kuna nini nikakuta watu wawili wanampiga risasi shemeji ikabidi nichukue stuli nikampiga mmoja akaanguka alafu nikaenda kuchukuq kisu nikamchoma nacho mwingine ndo wakachukuana wakaondoka"Amesema Salome Dady.

Nao baadhi ya majirani wameonyeshwa kuguswa na kusikitishwa na tukio hilo, awali kabla hawajaenda katika nyumba hiyo walisikia kelele ambazo walijua ni ugomvi wa kifamilia ndipo waliposikia sauti ya risasi wakafika eneo hilo ambapo walikuta watu hao wamekimbia baada ya kutenda tukio hilo.

Aidha Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga,ACP,Janeth Magomi Amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema cmJeshi la polisi linaendelea na msako wa kina kuwabainisha waliohusika na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso