MAHAKAMA YAAGIZA MWILI WA STELLA UFUKULIWE NA KUFANYIWA UCHUNGUZI MAJIBU YAPELEKWE MAHAKAMANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 19 December 2022

MAHAKAMA YAAGIZA MWILI WA STELLA UFUKULIWE NA KUFANYIWA UCHUNGUZI MAJIBU YAPELEKWE MAHAKAMANI


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni (Kinondoni) jijini Dar es Salaam imeamuru mwili wa mwanamke aliyefia mahabusu katika kituo cha Polisi Mburahati wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam, mwaka 2020, Stella Moses ufukuliwe na ufanyiwe uchunguzi kujua chanzo cha kifo chake.


Mahakama hiyo pia imeamuru matokeo ya uchunguzi huo yawasilishwe katika vyombo husika ili kama kuna watu waliohusika na kifo hicho wachukuliwe hatua za kisheria.


Uamuzi huo umetolewa leo Desemba 19, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu Franco Kiswaga, kufuatia maombi yaliyofunguliwa na wanafamilia wa marehemu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso