JESHI LA POLISI MKOA SHINYANGA LIMEKAMATA BUNDUKI AINA YA GOBOLE 01,BANGI NA VINGINEVYO. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 19 December 2022

JESHI LA POLISI MKOA SHINYANGA LIMEKAMATA BUNDUKI AINA YA GOBOLE 01,BANGI NA VINGINEVYO.

Katika kipindi cha kuanzia tarehe 22/11)2022 hadi 19/12/2022,Jeshi la polisi Mkoa Shinyanga limefanikiwa kukamata vitu na vielelezo mbalimbali kama ifuatavyo;(vifaa tiba ambavyo ni mali ya serikali,bunduki 01 ya kiraia aina ya gobole,simu janja 14,simu ndogo 3,pikipiki 10 za wizi zilizokuwa zikitumika kufanyia uhalifu,dawa za kulevya aina ya heroine kete 10,bangi kete 71,pombe haramu ya gongo lita 20,TV 04,na mitungi ya gesi 02.

RPC,Magomi akionyesha pikipiki walizozikamata ndani ya kipindi cha tarehe 22,11,2022 hadi 19,12,2022


NA HALIMA KHOYA,Huheso Digital SHINYANGA.


Akizungumza na vyombo vya habari leo Desemba 19,2022 kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga,ACP,Janeth Magomi,Akieleza kazi zilizofanywa katika operesheni na misako mbalimbali Amesema.


Magomi,Amesema katika kipindi hicho pia wamefanikiwa vyuma vya ujenzi wa minara ya TANESCO,Speaker 02,vitenge doti 04,compyuta 03,subwoofer 04,monitor 01,godoro 01,panga 01,shoka 01,na makabati 02 ya kuhifadhia chipsi.


"Lakini pia tuliokota pikipiki 08 na baiskeli 11 ambazo katika mazingira tofauti zilisahauliwa na wamiliki wake maeneo mbalimbali au kutupwa kutokana na sababu tofauti kama ulevi na mambo mengine kama hayo"Amesema Magomi.


Aidha katika kipindi hicho ,kesi mbalimbali ziliweza kufanikiwa mahakamani ambazo ni unyang'anyaji wa kutumia nguvu kesi 01,mauaji 03,kubaka 08,kulawiti 3,ukatili dhidi ya mtoto 02,kujeruhi 02,kuvunja nyumba usiku na kuiba 01,kupatikana na bangi 03,wizi wa mtoto 01,kupatikana na pombe ya moshi 02,kupatikana na mirungi 01,kumtorosha mtoto 01,kumpa mimba mwanafunzi 01,wizi 01 na wizi wa kuaminika ambapo kesi zote zilisikilizwa katika mahakama zote na kutolewa hukumu.


"Upande wa usalama barabarani kwa kipindi hicho hakukuwa na tukio lolote kubwa la barabarani japokuwa kulikuwa na makosa madogo madogo(Jumla ya makosa ya magari yalikuwa. 2796 na makosaya pikipiki yalikuwa 937 na yote yalichukuliwa hatua za kisheria kwa kushirikiana na vyombo vingine kama MAHAKAMA,LATRA,TANROADS,BIMA,FIRE na MANISPAA"Ameongeza.


Aidha jeshi la polisi Mkoa Shinyanga linaendelea kuwaasa wananchi ,madereva na bodaboda kufuata sheria za nchi wakati wote na kutojihusisha na vitendo vya kiuhalifu kwa namna yoyote hususani kipindi hiki çha sikuku za krismas na mwaka mpya ambapo amebainisha kuwa Polisi wamejipanga kikamilifu kukabikianana vitendo vya uhalifu na wahalifu.

RPC Janeth Magomi akiwa anazungumza na vyombo vya habari asubuhi ya leo desemba 19,2022 wakati wa kuwasilisha kazi iliyofanywa na polisi kwa kipindi hicho.

Pikipiki zilizokamatwa kwenye oparesheni mbalimbali mkoani Shinyanga.

Baiskeli zilizookotwa na polisi katika operesheni za kipindi hicho.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso