BILIONI 800 ZAHITAJIKA KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI HESLB WAITWA KUJIELEZA BUNGENI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 1 November 2022

BILIONI 800 ZAHITAJIKA KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI HESLB WAITWA KUJIELEZA BUNGENI


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Stanslaus Nyongo amesema Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, (HESLB), inahitaji Sh800 bilioni ili iweze kutoa mikopo kwa wanafunzi wote waliodahiliwa kujiunga na vyuo vikuu.


Nyongo ametoa kauli hiyo leo Jumanne Novemba Mosi, 2022 wakati akichangia hoja ya wanafunzi wa elimu ya juu kukosa mikopo iliyotolewa na Mbunge wa Biharamulo (CCM) Ezra Chiwelesa.


Amesema vigezo vinavyotumika kutoa mikopo vinavyoelezwa na HESLB, vinachanganya kwamba wanatoa mikopo kwa wanafunzi wasio na uwezo na yatima.


Amesema asilimia 62 ya mikopo inayotolewa na HESLB imekuwa ikitoa kwa wanafunzi waliosoma masomo ya sanaa (arts) ambao wakimaliza wanakwenda mtaani kwa sababu ya ukosefu wa ajira na hivyo kutorudisha mikopo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso