NISHATI SAFI YA KUPIKIA KUTENGEWA BAJETI NA SERIKALI-RAIS SAMIA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 1 November 2022

NISHATI SAFI YA KUPIKIA KUTENGEWA BAJETI NA SERIKALI-RAIS SAMIA



Serikali imejipanga kutenga fedha kwa ajili ya uanzishwaji wa mfuko maalum kwa ajili nishati safi ya kupikia.


Fedha hizo zitaanza kutengwa katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha lengo likiwa kumtua mama mzigo wa kuni kichwani.


Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza uamuzi huo leo wakati wa kongamano la kitaifa la nishati safi ya kupikia linalofanyika jijini Dar es Salaam.


Amesema kama ambavyo aliweka lengo la kumtua mama ndoo kichwani ndivyo ambavyo nguvu itawekwa kwenye kumtua mama kuni kichwani kwa kumpa nishati safi ya kupikia.


Bila ya kutaja kiasi gani kitakachowekwa Rais Samia amesema hatua hiyo ya kuanzisha mfuko itasaidia kuwavutia wadau wa maendeleo kuona haja ya kutunisha mfuko huo.


Amesema, “Nikiwa Makamu wa Rais niliweka lengo la kumtua mama ndoo kichwani nina furaha kusema kwamba nimetimiza kwa asilimia 80, ukiacha hizi athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, ukame unaotuandama, upatikanaji wa maji umeshuka.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso