BIBI WA MBUNGE MWIJAGE ASAFIRISHWA KWA MSHIKAKI KUPELEKWA GEREZANI AOMBA KUUNDWA TUME YA UCHUNGUZI WA POLISI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 9 November 2022

BIBI WA MBUNGE MWIJAGE ASAFIRISHWA KWA MSHIKAKI KUPELEKWA GEREZANI AOMBA KUUNDWA TUME YA UCHUNGUZI WA POLISI


Mbunge wa Muleba Kaskazini (CCM), Charles Mwijage ameomba Serikali kuunda tume ya kuchunguza tabia ya Polisi kukwepa gharama za kusafirisha mahabusu.


Mwijage ameliambia Bunge leo Jumatano Novemba 9, 2022 wakati akiuliza swali la nyongeza kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Mbunge huyo amesema majibu ya Serikali kuwa gharama hizo zinabebwa na watu wa Magereza na mahakama hazina uhalisia na hali ilivyo kwenye maeneo mengi.


"Mwaka jana bibi yangu Juliana Gaesha alikamatwa na kupelekwa Kamachumu lakini ambapo alihukumiwa kifungo lakini Wakati anatoka mshtaki wake alitakiwa kulipia gharama na walibebwa mishikaki,"amesema Mwijage.


Katika swali la msingi mbunge huyo ameomba kujua nani anatakiwa kuwagharamia watuhumiwa wa uharifu wanapokuwa chini ya Polisi hasa wanapotakiwa kwenda mahakamani.


Akijibu maswali hayo kwa pamoja, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini amesema jukumu la kugharamia watu hao ni la vyombo husika ikiwemo Polisi na Magereza.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso