WATOTO WAWILI WAFARIKI KWA AJALI YA GARI MKOANI MBEYA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 9 November 2022

WATOTO WAWILI WAFARIKI KWA AJALI YA GARI MKOANI MBEYA

Watoto wawili wa familia moja wamepoteza maisha papo hapo kwenye ajali iliyohusisha magari matatu iliyotokea leo Jumatano Novemba 9, 2022 katika mteremko wa Iwambi mkoani Mbeya.


Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea ajali hiyo akieleza chanzo ni mwendo kasi katika moja ya gari aina ya fuso.


"Katika ajali hiyo ni watoto wawili wa familia moja (waliokuwa katika gari dogo) wamepoteza maisha, niendelee kuwaomba madereva kuwa waangalifu wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto ili kuondokana na ajali hizi," amesema Kuzaga.


Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wamesema tukio hilo lilitokea saa 12 asubuhi ambapo dereva wa gari aina Costa alijitahidi kumudu gari lake lakini alishindwa baada ya kugongana ubavu na gari dogo.


Baraka Hamis, mkazi wa Mbalizi amesema akiwa na mwenzake muda huo wakifanya mazoezi ya viungo walishuhudia ajali hiyo lakini waliweza kusaidia kuokoa madhara makubwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso