MGANGA WA KIENYEJI KUNYONGWA MKOANI RUKWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 26 October 2022

MGANGA WA KIENYEJI KUNYONGWA MKOANI RUKWA


Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga imemhukumu mganga wa jadi, James Kapyela (57) kunyongwa hadi kufa, baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuwaua kwa makusudi watoto Nicholaus Mwambage (7) na Emmanuel Juma (4).


Ilidaiwa kuwa mganga huyo aliwalawiti watoto hao kabla ya kuwaua na kutupa miili yao kwenye pagala liliopo nyumbani kwake Machi 23, 2019 katika Mtaa wa Vuta, Kitongoji cha Kizwite, Sumbawanga Mjini.


Jaji Thadeo Mwenempazi alisema wakati akisoma hukumu hiyo jana Jumaamne Oktoba 25, 2022 kuwa mahakama imeridhika kuwa mashahidi 11 wa Jamhuri wamethibitisha mashtaka dhidi ya mganga huyo.


Jamhuri iliwakilishwa na mawakili Marieta Maguta waliosaidiana na wakili Saimon Peres.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso