WAKULIMA WAIOMBA SERIKALI MBOLEA,WAAHIDI KUBORESHA SEKTA YA KILIMO,SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 26 October 2022

WAKULIMA WAIOMBA SERIKALI MBOLEA,WAAHIDI KUBORESHA SEKTA YA KILIMO,SHINYANGA

Baadhi ya wakulima wa Kata ya Mwawaza katika halmashauri ya manispaa ya shinyanga Mkoani Shinyanga wamelalamikia ucheleweshwaji wa namba za kuchukulia mbolea ya ruzuku iliyotolewa na serikali hali inayopelekea kushidwa kufanya shughuli za kilimo.

Mbolea


NA HALIMA KHOYA,SHINYANGA


Malalamiko hayo yametolewa Oktoba 24,mwaka huu na baadhi ya wakulima hao wa kata ya mwawaza Manispaa ya Shinyanga Mkoani humo.


Akieleza juu ya adha hiyo Mmoja wa wakulima hao,Malunde Daud amesema licha ya wao kujiandikisha ili kupokea Ruzuku hiyo bado wanakabiliwa na changamoto ya kucheleweshwa kwa namba za kuchukua mbolea kutoka kwa wakala anayehusika na usambazaji wa mbolea hiyo.



Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo,Juma Nkwabi amesema kata hiyo inazungukwa na asilimia kubwa ya wakulima hivyo anaiomba serikali kuongeza kasi katika zoezi la utoaji wa mbolea hiyo ili wakulima hao waweze kuendesha shughuli zao kwa wakati.


"Kimsingi Kata hii ni kubwa ambapo inazungukwa na asilimia kubwa ya wakulima ningependa sana kuiomba serikali wajaribu kuangali kwa kuanzia tukipata tu walau tani 80 au 100 ili ziweze kukidhi mahitaji ya wananchi"Amesema Nkwambi.


Nae afisa kilimo Manispaa ya Shinyanga, Erasto Protas amesema bado kuna changamoto kubwa katika utoaji wa ruzuku ya mbolea hiyo kwani baadhi ya wakulima bado hawana elimu juu umuhimu wa kutumia mbolea katika zoezi zima la kilimo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso