WALIONDOLEWA KAZINI KUREJESHEWA MICHANGO YAO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 26 October 2022

WALIONDOLEWA KAZINI KUREJESHEWA MICHANGO YAO

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameridhia kuwa watumishi wote walioondolewa kazini kwa kughushi vyeti warejeshewe michango yao tu waliyokatwa kwenye mishahara na kuwasilishwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kuidhinisha shilingi Bilioni 46.89 zilipwe kundi hilo.



Akitoa maamuzi hayo ya Rais kwa niaba ya serikali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako ameagiza mifuko ya hifadhi ya Jamii ya PSSSF na NSSF iangalie utaratibu mzuri wakurejesha michango ya wafanyakazi iliyowasilishwa kwenye mifuko hiyo bila kuhusisha michango ya mwajiri na zoezi hilo la marejesho ya michango ya watumishi hao yataanza Novemba 1, 2022.


Kuhusu watumishi waliofariki na wanapaswa kurejeshewa michango yao Prof. Ndalichako ameelekeza wale waliooandikwa kwenye urithi wafanye utaratibu wakupata fedha hizo, huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama ameagiza waajiri wote wazingatie maadili ya watumishi wa umma katika utoaji wa fedha hizo na kusiwe na mianya ya rushwa kwani kila hatua serikali inafwatilia na atakayebainika kukiuka maelekezo ya serikali atachukuliwa hatua za kinidhamu.


Malipo hayo yanakuja baada ya shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kupitia risala yao wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei mosi kumuomba Rais Samia aangalie namna ya kuwafuta jasho watumishi hao.

CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso