AFUNGWA MAISHA KWA UBAKAJI WA MTOTO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 20 October 2022

AFUNGWA MAISHA KWA UBAKAJI WA MTOTO


Mahakama ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa imemhukumu kifungo cha maisha jela mfanyabiashara wa mjini Namanyere, Athanas Exavery (32) baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike wa miaka saba.


Akitoa hukumu hiyo leo Alhamisi Oktoba 20, 2022 Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa mahakama Hhiyo, Denis Luwungo amesema kuwa mahakama imemkuta na hatia mtuhumiwa chini ya kifungu cha 130 (1) cha 2 (e) na kifungu cha 131 (3) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16.


Amesema kuwa mahakama imejiridhisha pasipo shaka kwamba baada ya upande wa mashitaka kuleta ushahidi wa mashahidi sita na vielelezo sita na kumkuta na hatia hivyo imemhukumu kifungo cha maisha jela.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso