BREAKING: IGP WAMBURA AMNG'OA BARABARANI MTAFUNGWA AMPELEKA MWANZA KUWA RPC - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 20 October 2022

BREAKING: IGP WAMBURA AMNG'OA BARABARANI MTAFUNGWA AMPELEKA MWANZA KUWA RPC

IGP WAMBURA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillus Wambura amewahamisha baadhi ya Makamanda wa Polisi kutoka katika nafasi zao na kuwapangia sehemu nyingine.
kamanda Mtafungwa aliekuwa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani nchini

Amempangia Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei kuwa Mkuu wa Kitengo cha Polisi Wasaidizi na Kampuni Binafsi za Ulinzi nchini ambapo anachukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Issack Katamiti.


Pia, amewahamisha Ramadhani Ng'anzi aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza kwenda kuwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania na aliyekuwa Mkuu wa Kikosi hicho Wilbroad Mutafungwa anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.


Aidha aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Kipolisi Rufiji Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Protus Mutayoba, amekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rufiji baada ya Kamanda wa Mkoa huo kuhamishiwa Mkoa wa Kipolisi Temeke hivi karibuni.

Chanzo:Millardayo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso