SABAYA NA WENZAKEWAFIKISHWA MAHAKAMANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 29 August 2022

SABAYA NA WENZAKEWAFIKISHWA MAHAKAMANI



Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, kwa ajili ya kusikiliza kesi inayowakabili.


Sabaya na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumatat, Agosti 29, 2022 ambapo wanakabiliwa na mashitaka saba ikiwamo la uhujumu uchumi, kuongoza genge la uhalifu pamoja na kujihusisha na vitendo vya rushwa.


Juni Mosi, 2022, Sabaya na wenzake wanne walipandishwa mahakamani hapo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kusomewa mashtaka yanayowakabili mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha.


Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni, Sylvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey.







No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso