SENSA YA WATU NA MAKAZI YAONNGEZWA SIKU SABA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 29 August 2022

SENSA YA WATU NA MAKAZI YAONNGEZWA SIKU SABA

Kamisaa wa sensa ya watu na makazi Anna Makinda amesema hadi kufikia saa mbili asubuhi ya leo kaya zilizohesabiwa ni asilimia 93.45 na hivyo wameamua kuongeza muda wa ziada wa siku 7 kukamilisha zoezi hilo.

Kamisaa wa sensa ya watu na makazi Anna Makinda


Makinda amesema katika siku hizo mwananchi ambaye hajahesabiwa atapatiwa namba ya simu ambayo atapiga na kutoa taarifa zake kuanzia kesho.Amewataka wananchi ambao hawajahesabiwa katika zoezi hilo kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa makarani wa sensa watakaokuwa wanazungumza nao kwa njia ya simu ili kutoa taarifa zao.


Katika hatua nyingine Kamisaa huyo wa sensa ya watu na makazi ametangaza kuanza sensa ya majengo nchi nzima ambayo itaanza mara tu baada ya kukamilika kwa zoezi la sensa ya watu na makazi.


Akizungumzia changamoto zilizojitikeza wakati wa zoezi hilo ikiwemo vishkwambi kuisha umeme na baadhi ya makarani na wajumbe wa mtaa kutolipwa posho zao mkurugenzi wa huduma za sensa amesema hakuna mtu ambaye hatalipwa.

Chanzo:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso