RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA MKOANI TANGA HIKI NDIO ATAKIFANYA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 13 August 2022

RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA MKOANI TANGA HIKI NDIO ATAKIFANYA

RAIS Samia Suluhu anatarajiwa kuwasili kesho mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya siku mbili mkoani Tanga ambapo akiwa mkoani hapa atazindua Chuo cha Jeshi la Uhamiaji cha Taifa.


Akizungumza leo wakati wa halfa ya kukabidhiwa ofisi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba alisema Rais Samia ataingia mkoani Tanga kesho mchana na Jumatatu atafanya ziara wilayani Mkinga.


Mgumba alisema Rais Samia atazindua chuo hicho cha Jeshi la Uhamiaji kilichojengwa eneo la Boma KichakaMiba wilayani Mkinga ikiwemo kufunga mafunzo ya wanajeshi wa jeshi jipya la Uhamiaji zaidi ya 818 waliohitimu mafunzo.


Alisema baada ya Rais Samia ataondoka ambapo pia alitoa rai kwa wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kumlaki katika maeneo yote atayopita.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso